Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
Vimondo (pia: meteori au meteoridi) ni magimba madogo ya angani yanayozunguka jua. Yanaweza kuangukia duniani yakionekana kama moto angani. Ukubwa wa kimondo ni kuanzia punje ya mchanga hadi kufikia kipenyo cha mita kadhaa. Hivyo kimondo ni kidogo kuliko asteoridi na kikubwa kushinda vumbi la angani. Obiti ya kimondo inaweza kuingiliana na obiti ya dunia au sayari nyingine. Kimondo kikilikaribia gimba la angani kubwa zaidi kinavutwa nalo.
Kikikaribia mno dunia yetu kinaingia katika angahewa na kuanguka chini kwa kasi kubwa sana. Njiani kinapashwa moto kutokana na shindikizo la hewa dhidi yake. Kiasi cha joto kinatosha kuchoma kabisa kimondo kidogo hewani. Hii inaonekana kwa macho matupu kama mstari wa moto angani. Kama kimondo ni kikubwa zaidi ni sehemu zake za nje tu zinazochomwa na kiini kinagonga uso wa dunia.
Kati ya vimondo kumi vikubwa kabisa duniani ambavyo mabaki yake yanaonekana, kimojawapo ni Kimondo cha Mbozi nchini Tanzania. ►Soma zaidi
Picha nzuri ya wiki
Ziara ya Mwalimu Nyerere wa Tanzania mnamo Machi 12, 1985; Rais Nyerere akisikiliza maswali.
Julius Nyerere (Butiama, 13 Aprili 1922 - London, 14 Oktoba 1999) alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania na Baba wa Taifa. Aliongoza Tanganyika tangu uhuru mwaka 1961 kama Waziri Mkuu, kisha baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, aliongoza Tanzania kama Rais hadi 1985. Aliunda sera ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo iliweka msisitizo kwenye usawa wa kijamii, elimu kwa wote na umoja wa kitaifa. Baada ya kustaafu urais, aliendelea kuishi kwa kuendeleza shughuli za kijamii na kilimo, na alifariki dunia kutokana na saratani ya damu tarehe 14 Oktoba 1999 akiwa London, na kuzikwa Butiama. Je ungependa kusoma zaidi kuhusu Mtu huyu? au ungependa kuchangia zaidi kuhusu mtu huyu? fungua Hapa
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
Idadi ya makala: 102,872
Idadi ya kurasa zote: 207,112 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
Katika mwezi wa Agosti 2025 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 7.79 hivi, ambayo ni sawa na mara 251,607 kwa siku au mara 10,483 kila saa ambalo ni ongezeko la mara 4.5 ukilinganisha na mwaka 2024 mwezi wa Agosti. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
(fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
(unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya Shirika Lisilo la Kiserikali la Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.